GADIEL Michael, beki wa timu ya Simba amesema kuwa bado ana nafasi ya kufanya makubwa ndani ya Simba kutokana na uwezo alionao.
Gadiel alisajiliwa na Simba kwenye dirisha kubwa la msimu wa 2019/20 akitokea Yanga ambapo akiwa Simba amecheza mechi nane ambazo ni sawa na dakika 720 hku akikosekana kwenye mechi 20 ambazo ni sawa na dakika 1,800.
Vita yake kubwa ndani ya Simba ni dhidi ya Mohamed Hussein,’ Tshabalala’, kwa wakati huu wa mapumziko kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona amesema amepewa program na Kocha Mkuu Sven Vanderbroek jambo analoamini litamrejesha kwenye ubora.
"Sina tatizo na uwezo wangu na ninajua kwamba bado nafasi ipo ya kurejea kwenye ubora, kikubwa ni kujituma na kuendelea kufanya mazoezi, ishu ya namba ipo chini ya mwalimu ila bado ninafanya mazoezi kwa sasa kujiweka fiti," amesema.
Simba imejikusanyia pointi 71 kibindoni na inaongoza Ligi Kuu Bara na imefunga mabao 63.
Post a Comment