ABDI Banda, nyota wa Tanzania anayekipiga Klabu ya Highlands Park inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini amesema kuwa kwa sasa anaendelea kupiga matizi ili kujiweka sawa licha ya ligi kusimama kwa muda kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.
Highlands Park ipo nafasi ya nane katika Ligi Kuu ikiwa imecheza mechi 24 na kibindoni ina pointi 31.
Banda ambaye ni beki amesema:"Nipo salama na ninaendelea vizuri huku, kikubwa ambacho tunakifanya kwa sasa tukiwa wachezaji wa timu ni kuhakikisha kwamba kila mmoja anafanya mazoezi akiwa nyumbani ili kulinda kipaji chake.
"Tumepewa programu maalumu na benchi la ufundi ambalo linatufuatilia mipango yetu na namna ambayo tunafanya katika kipindi hiki," .
Post a Comment