SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kama nyota wake wanaokosa namba kikosi cha kwanza wanataka kuanza lazima wapambane mazoezini kuwa bora.

Kauli hiyo inawagusa nyota wengi ndani ya Simba ambao hawana nafasi kikosi cha kwanza ikiwa ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Haruna Shamte, Said Ndemla, Yusuph Mlipili na Rashid Juma ambao wamekuwa wakisugua benchi muda mwingi.

Sven amewataka wachezaji wake kujituma ili waweze kuwa bora muda wote ndani ya uwanja. 


"Sina tatizo na mchezaji yoyote ndani ya Simba lakini ikumbukwe kuwa nina wachezaji wengi ambao wapo na wana uwezo mkubwa jambo hilo linanifanya niwape nafasi.

"Ili wachezaji wengine waweze kupata nafasi ni lazima waongeze juhudi kwenye mazoezi kwa kufanya kwao vizuri huko kutanifanya niwape nafasi ya kucheza," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.