HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa mashabiki wanahitaji ushindi muda wote bila kujali kama wakati mwingine wachezaji wanapita kwenye kipindi kigumu jambo linalowafanya wapambane kutafuta matokeo.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa wamekuwa wakipambana wakiwa uwanjani kwa hali na mali kwani wanatambua mashabiki wanahitaji ushindi.
"Mashabiki wao uhitaji wao ni kuona timu ikiwa uwanjani inapata matokeo bila kujali hali za wachezaji wapo katika wakati gani, muda mwingine unaweza ukawa unaingia kucheza lakini una matatizo yako ya kifamilia hakuna anayejali.
"Hali hiyo inatufanya nasi kutumia nguvu nyingi kutafuta matokeo ndani ya uwanja kikubwa ni kuwapa furaha mashabiki na kutimiza kazi yetu, matatizo yapo sasa yanapotokea ni lazima ujue namna ya kupambana nayo kwani kazi nayo ni muhimu" amesema.
Post a Comment