PIERRE-Emerick Aubameyang, nahodha wa kikosi cha Arsenal kilicho chini ya Kocha MKuu, Mikel Arteta inaonyesha kuwa hana nia ya kubaki ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu England.
Imeripotiwa kuwa mabosi wa Manchester United wameingia kwenye anga za kuiwinda saini yake huku Barcelona pia wakihusishwa kumtaka raia huyo wa Gabon anayekipiga pia kwenye timu yake ya Taifa.
Kwenye video waliyokuwa wakiwasiliana na rafikiye Kevin-Prince Boateng ambaye ni kiungo raia wa Ghana alipoulizwa kuhusu mkataba wake ndani ya Arsenal, Auba alisema kuwa amebakiza mwaka mmoja na alipotakiwa kufafanua kama atabaki ndani ya kikosi hicho hakuwa tayari zaidi ya kucheka na kusema hakikahakika.
Mghana huyo alimwambia kuwa mashabiki wanatambua kwamba amepata dili jipya nje ya Arsenal jambo ambalo halikupingwa na nahodha huyo aliyesema kuwa analitambua hilo.
Arteta amesema kuwa bado wanahitaji huduma ya nyota huyo wanaendelea kuzungumza naye wanauhakika kila kitu kitakuwa sawa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.