JACKSON Mayanja aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC ametwaa tuzo ya Kocha Bora kwa mwezi Februari akiwa na kikosi cha KFC cha Uganda.
Kocha huyo aliingia mkataba na timu hiyo mara baada ya kupigwa chini ndani ya KMC.
Mayanja amekiongoza kikosi hicho kutoka kwenye nafasi ya 16 hadi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uganda pia amefanikiwa kukifikisha Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho nchini Uganda.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mayanja amesema kuwa kikubwa ni nafasi ya kuaminiwa na kusimamia majukumu kwa wakati jambo lililompa nafasi ya kufanya vizuri.
"Nimekuwa nikipewa nafasi ya kukiongoza kikosi kwa uhuru jambo ambalo limenipa uwezo wa kuwaongoza vijana kufanya vizuri," amesema.
Kwa sasa Ligi ya Uganda imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali ya Uganda imechukua tahadhari kwa kuzuia mijumuiko isiyo ya lazima.
Post a Comment