WILLIAM Lucian ‘Gallas’, beki wa Polisi Tanzania, amesema kuwa anatumia muda mkubwa kufanya mazoezi ili kuwa fiti endapo Ligi Kuu Bara itarejea.

Kwa sasa ligi imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ilitoa tamko Machi 17 kusimamisha mijumuiko yote isiyo ya lazima.

Akizungumza na Saleh Jembe, Gallas amesema kuwa ni muhimu kwa kila mchezaji kufuata programu aliyopewa ili kuwa imara.

"Ninafanya mazoezi ili kulinda kipaji changu nina amini hata wachezaji wengine wanafanya pia ni muhimu kwa afya na kipaji pia.

"Virusi vya Corona vipo ni muhimu kuchukua tahadhari ili kuwa salama kwani afya ni utajiri mkubwa mengine yanafuata," amesema.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 29 safu yao ya ulinzi imeruhusu mabao 26 na ina pointi 45 kibindoni. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.