BERNARD Morrison, Kiungo Mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kabla ya kutua Bongo alipata ofa nyingi Afrika Kusini pamoja na Ghana ambapo ndipo maskani yake ilipo.
Morrison ni ingizo jipya ndani ya Yanga alisajiliwa akiwa mchezaji huru na miongoni mwa timu ambazo alizicheza ni pamoja na Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
"Nilikuwa na ofa nyigi mkononi kutoka timu mbalimbali ikiwa ni pamoja na zile za nyumbani Ghana, Afrika Kusini na Ulaya ila zote niliamua kuziacha ili nije Bongo ambapo nipo kwa sasa kwa sababu nilipenda kupata changamoto mpya nje ya Afrika Kusini.
"Mwanzo nilikuwa ninataka kwenda Afrika Kusini lakini nikaona ni bora nije hapa ndani ya Yanga ambapo nipo kwa sasa na maisha yanaendelea," amesema.
Morrison amecheza mechi 10 za Ligi Kuu Bara ndani ya Yanga ametupia mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.
Post a Comment