BAKARI Nondo, beki chipukizi anayekipiga ndani ya Coastal Union na pia ana nafasi ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Tafa Starsinaelezwa kuwa yupo kwenye rada za uongozi wa Simba ili akaongeze nguvu kwenye kikosi hicho cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Nondo anavaa kitambaa cha unahodha ndani ya Coastal Union iliyo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda licha ya kuwa beki ametupia bao moja kati ya 27 ambayo yamefungwa na Coastal Union.

Habari zinaeleza kuwa tayari kila kitu kinakwenda sawa ni suala la muda tu beki huyo kuibuka Msimbazi kuungana na Pascal Wawa.

"Kila kitu kipo sawa kwani dau limeandaliwa ili kumpata beki huyo kwa kuwa ana vigezo ambavyo Kocha Mkuu Sven anavitaka," ilieleza taarifa hiyo.

Simba ikiwa imecheza mechi 28 safu yake ya ulinzi imeruhusu mabao 15 ya kufungwa ikiwa ni ya kwanza kufungwa mabao machache inayofuata ni Coastal Union ambayo imecheza mechi 28 imefungwa mabao 19.

Katibu Mkuu wa Simba, Dk. Arnold Kashembe amesema kuwa masuala ya usajili bado kuanza kuyazungumzia kwa sasa.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.