IBRAHIM Ajibu kiungo mshambuliaji ndani ya Simba amecheza mechi 16 ambazo ni dakika 1,440 kati ya 28 ambazo ni dakika 1,520 ambazo wachezaji wa Simba wamezitumia uwanjani kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

Alianza kikosi cha kwanza mechi 11 ambazo ni dakika 990 na kuanzia benchi mechi tano ambazo ni dakika 450.

Ametumia jumla ya dakika 948 uwanjani na ametoa pasi nne za mabao na kufunga bao moja dhidi ya Polisi Tanzania. Ajibu ana wastani wa kutiumia dakika 59 kwenye mechi zake za ligi ndani ya Simba na amekosekana kwenye mechi 12 ambazo ni dakika 1,080.


Yeye ni miongoni mwa supersub ndani ya Simba kwani bao lake aliifunga Polisi Tanzania Uwanja wa Taifa akitokea benchi na alichukua nafasi ya Sharaf Shiboub.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.