HIMID Mao, kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga nchini Misri kwenye Klabu ya ENPPI amesema kuwa anaendelea salama.
Ligi Kuu ya nchini Misri imesimama ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo ni janga la dunia kwa sasa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Himid amesema kuwa wanashinda ndani kutokana na katazo la Serikali kutowapa ruhusa kutoka nje.
"Tunaendelea salama huku licha ya kwamba hatuna nafasi ya kutoka nje kama zamani, mazoezi na shughuli nyingine tunafanyia ndani," amesema Himid.
Post a Comment