PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa nafasi waliyoachwa na Simba kuwafikia kwa sasa kunahitaji juhudi na akili nyingi kutokana na mzigo wa pointi wanazodaiwa na idadi ya mechi walizonazo.
Tshishimbi amesema ni ngumu kuifikia Simba kwa sasa kwa pointi labda itokee wapoteze mechi zao zilizobaki na wao washinde mechi zao zilizobaki jambo ambalo anaona ni mtihani mgumu kufanikiwa hivyo amekubali yaishe kwa upande wa ubingwa.
Yanga ipo nafasi ya tatu na pointi 51, tofauti ya pointi 20 na Simba yenye pointi 71. Yanga imebakiwa na mechi 11, Simba mechi kumi.
“Haitakuwa kazi rahisi kuyafikia malengo ya kutwaa ubingwa kutokana na mambo yalivyo kwa sasa ila inaweza kutokea kutokana na mchezo wa mpira kuwa na matokeo tofauti labda ikishindikana sasa itakuwa wakati ujao.
"Wapinzani wetu wametuacha kwa pointi nyingi hilo linatoa nafasi kwao kutwaa ubingwa tena labda sisi tujipange kwa wakati ujao," amesema.
Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimama kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea baada ya mwezi mmoja.
Post a Comment