BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amefunguka kuwa kuifungia timu yake bao mbele ya Simba kumempa heshima na furaha kwa mashabiki wa Yanga.
Raia huyo wa Ghana alifunga bao hilo kwenye mchezo wake wa kwanza wa dabi uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa na Yanga ilishinda bao 1-0.
Morrison amehusika kwenye mabao sita kati ya 31 ya Yanga ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.
"Furaha kubwa niliona kwa mashabki namna walivyofurahi na namna walivyonipokea hakika ilikuwa ni siku nzuri kwangu, wachezaji wenzangu na mashabiki kiujumla.
"Ninaona kwamba kila shabiki anapenda kupata matokeo mazuri lakini hayaji bila kushirikiana na kufanya yote kwa upendo hvyo wazidi kuwa pamoja nasi kila wakati," amesema.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Post a Comment