GERAD Mdamu, mshambuliaji wa Mwadui FC kwa sasa amejichimbia mkoani Dodoma akiendelea kunoa kiwango chake wakati huu Ligi Kuu Bara ikiwa imesimamishwa kutokana na kupambana na maambukzi ya Virusi vya Corona.
Mdamu ana mabao manne ndani ya ligi ambapo bao lake la mwisho aliifunga Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Kambarage ambao Mwadui ilishinda kwa bao 1-0 na pia aliitungua Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambapo Simba ilipenya hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa kwa sasa amejichimbia Dodoma huku akichukua tahadhari ya Virusi vya Corona pamoja na kuendelea kulinda kiwango chake kwa kufanya mazoezi.
"Nipo Dodoma kwa sasa ninachukua tahadhari juu ya Virusi vya Corona kwani afya ni muhimu, pia ni balozi kwa wengine kuhusu namna ya kujilinda kwa vile ninavyoelewa pamoja na kufuatilia taarifa kwenye vyombo vya habari.
"NInaendelea pia na mazoezi ili kujiweka sawa kwani kikubwa ni kulinda kipaji changu kwa manufaa yangu na timu kiujumla,' amesema.
Mwadui FC ipo nafasi ya 12 ikiwa imecheza mechi 28 na kibindoni ina pointi 34.
Post a Comment