KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola amesema kuwa ni muhimu kwa wachezaji kufuata program walizopewa ili kulinda vipaji vyao.

Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda wa mwezi mmoja na Serikali ya Tanzania ili kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona na wachezaji wengi wamepewa mapumziko.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa kwa sasa ni muhimu wachezaji kufuata program ambazo wamepewa na makocha wao.

"Wakati huu wachezaji wapo kwenye mapumziko kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corna ni muhimu kwao kufuata program ambazo wamepewa na mwalimu ili kulinda vipaji vyao.

"Wakati wa sasa ni mgumu kwani kukaa bila kufanya mazoezi kwa mchezaji ni hatari iwapo watafuata programu itakuwa afya kwao na kwa timu pia," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.