PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli amesema kuwa anaweza kikubwa kilicho nyuma ya mafanikio yake ni kuamini uwezo wake na kujituma.
Nonga ndani ya Ligi Kuu Bara amefunga mabao 11 na kutoa pasi nne za mabao ambapo ni miongoni mwa wazawa wenye mabao mengi huku wengine wakiwa ni Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar na Reliants Lusajo wa Namungo FC.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa:-"Nina uwezo mkubwa na kipaji ninacho kutokana na kupenda kile ambacho ninakifanya, hicho kinanipa nguvu ya kufanya vizuri.
"Kwa sasa ligi ikiwa imesimama bado tunaendelea kujipanga ili kuwa bora kwani kwa sasa ukitulia itakuwa ngumu kurudi kwenye ubora," amesema.
Lipuli ipo nafasi ya 13 ikiwa imecheza mechi 29 ina pointi 33 kibindoni.

Post a Comment