KATIKA kukiboresha kikosi chao, uongozi wa Simba umeahidi kutomuachia mchezaji yeyote watakayemuhitaji kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu zienee tetesi za viungo wao, Mzambia Clatous Chama na Mkongomani, Deo Kanda saini zao kuwaniwa na watani wao wa jadi, Yanga.
Nyota kadhaa wa Simba mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu akiwemo Yusuf Mlipili, Hassani Dilunga, Paul Bukaba, Mohammed Ibrahim na Deo Kanda anayecheza hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe. Chama mkataba wake umebaki mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, uongozi wa timu hiyo umetenga fedha ili kuhakikisha wachezaji wanaomaliza mikataba yao Nyota kadhaa wa Simba mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu akiwemo Yusuf Mlipili, Hassani Dilunga, Paul Bukaba, Mohammed Ibrahim na Deo Kanda anayecheza hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe.
Post a Comment