HARRY Kane amesema kuwa anaamini yupo fiti kwa sasa kurejea uwanjani iwapo Ligi Kuu England itarejea.

Kane anayekipiga Klabu ya Tottenham alikuwa nje Kwa muda baada ya kufanyiwa upasuaji Januari mwaka huu ameshaanza mazoezi mepesi kujiweka fiti.

Ligi Kuu ya England inatarajia kurejea Aprili 30 kutokana na kusimama kwa muda kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Kurejea kwa nyota huyo kutampa tabasamu Kocha Mkuu, Jose Mourinho ambaye amekuwa akilalamika kukosa washambuliaji.


 "Naamini sipo mbali na kurejea uwanjani, matumaini yangu nitarejea wiki mbili kama siyo tatu zijazo," amesema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.