NCHIMBI NYOTA WA YANGA ASEPA DAR MAZIMA NA KUIBUKIA KIJIJINI KUENDELEA NA MAISHA
DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kutokana na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona ameamua kusepa ndani ya Dar es Salaam na kuibukia kijijini kwao Songea.
Nchimbi alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Polisi Tanzania ambapo alikuwa akicheza kwa mkopo alikopelekwa na mabosi wake Azam FC.
Kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona Ligi Kuu Tanzania Bara imesimamishwa na inatarajiwa kurejea baada ya siku 30.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nchimbi amesema kuwa ameamua kwenda kijijini ili kutoa somo kuhusu Virusi hivyo na kupata muda wa kupumzika.
"Kwa sasa sipo Dar nipo zangu Songea huku kijijini kwetu ambapo nimekuwa nikichukua tahadhari ya Virusi vya Corona pamoja na kutoa elimu kwa familia namna ya kujilinda.
"Kiukweli hali sio shwari maana mpaka ligi imesimama mambo sio ya kuchukulia utani, muhimu kufuata kanuni na utaratibu ambao tumekuwa nao tuuboreshe zaidi, " amesema Nchimbi.
Ndani ya Ligi Kuu Bara, Nchimbi ana mabao sita ambapo alifunga mawili akiwa na Yanga na alifunga manne akiwa ndani ya Polisi Tanzania.
Post a Comment