ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA, JAKSON MAYANJA AWAPA MAJUKUMU WACHEZAJI WAKE
JAKSON Mayanja, aliyekuwa Kocha Mkuu wa KMC, Kagera Sugar, Coastal Union na Simba amesema kuwa kutokaana na kusambaa kwa Virusi vya Corona amewataka wachezaji wake kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za afya ili kuwa salama na familia zao.
Mayanja alipewa kandarasi ya mwaka mmoja ndani ya KMC iliyokuwa na kipengele cha kuongeza mkataba msimu huu wa 2019/20 hakudumu kutokana na matokeo mabovu na kwa sasa yupo nchini Uganda akiwa na kikosi cha Kyetume FC.
"Virusi vya Corona sio vya kuchukulia utani ni lazima wachezaji wajilinde na wachukue tahadhari nimewaambia kwamba wakiwa nyumbani ni lazima walinde familia zao na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine, pia nimewaambia wasisahau kufanya mazoezi.
"Nimewapa programu ambazo wataweza kuzifanya wakiwa nyumbani bila bugudha hata na wake zao pia kwani mazoezi ni ya wote," amesema.
Post a Comment