NYOTA wa Atletico Madrid, Kieran Trippier amefunguka kuwa anatamani siku akistaafu soka basi arudi kuichezea timu yake ya zamani ya Burnley.
Beki huyo alijiunga na Atletico majira ya joto mwaka 2019 na ni msimu wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo.
Trippier amesema kuwa anatamani kustaafu masiaha ya soka akiwa ndani ya timu yake ya zamani ambayo aliitumikia zamani.
“Natamani kustaafu soka langu nikiwa katika klabu ya Burnley, nataka kucheza kwa kiwango ili ukifika muda wa kuondoka basi Burnley ndiyo timu sahihi kwangu kumalizia soka.
Post a Comment