NYOTA wa Simba, Sharraf Eldin Shiboub, Mzamiru Yassin ambao ni viungo na beki wa kati Pascal Serge Wawa wameitwa mezani ili kumalizana na Simba.

Nyota hao kandarasi zao zipo ukingoni na mwishoni mwa msimu zinakamilika jambo linalotoa ruhusa kwa mabosi wa Simba kuzungumza na wachezaji hao.

Sharaf amekuwa akitimiza majukumu yake ndani ya Simba ambapo amefunga mabao mawili na kutoa pasi sita za mabao huku Mzamiru licha ya kutoonekana ndani ya uwanja baada ya mechi ya watani Januari 4 mguuni ana pasi tatu za mabao.

Wawa yeye amekuwa ni tegemeo kwa mabeki licha ya kuwa ni beki amehusika kwenye pasi moja ya bao lililofungwa na Meddie Kagere naye pia ameitwa mezani.

Habari zinaeleza kuwa nyota hao wamepitishwa na Kocha Mkuu Sven Vandernbroeck ili kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Nyota hao kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ni wachezaji wanaoruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine itakayowahitaji kutokana na kubakisha miezi sita katika mikataba yao.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.