AHMAD Kassim ‘Prezdaa’, Meneja wa Mshambuliaji wa Namungo, Reliants Lusajo amesema kuwa wapo tayari kufanya kazi na Yanga kama watamhitaji mchezaji wake.
Lusajo ambaye ni nahodha wa Namungo amehusika kwenye mabao 14 ya Namungo ametupia mabao 11 na kutoa asisti tatu.
Ahmad amesema Lusajo amebakiza kandarai ya miezi mitatu jambo linalotoa nafasi ya kuzungumza na timu yoyote inayohitaji saini yake.
“Miezi mitatu ya mkataba wake na Namungo inampa fursa ya kufanya mazungumzo na kutua klabu yoyote ile hata iwe Yanga hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni makubaliano tu ila kipaumbele kikubwa ni Namungo,".
Lusajo aliwahi kutumika ndani ya Yanga ila hakuweza kutakata kwa sasa ameibukia Namungo ambapo amepewa na kitambaa cha unahodha.
Post a Comment