KOCHA wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Ronald Koeman amesema sio mbaya ikitokea siku moja akaja kuifundisha Barcelona sababu ni timu bora.
Koeman alisema Barca imetwaa makombe makubwa jambo ambalo kila kocha anaweza kutamani timu ya namna hiyo.
“Barca ni timu nzuri, inawachezaji wazuri na una uwezo wa kusajili mchezaji unayemtaka hivyo lazima upende timu ya namna hiyo,”alisema Koeman.
Kwa sasa Barcelona inatajwa kuwinda saini ya kiungo wa Manchester United Paul Pogba ili kupata huduma yake.
Post a Comment