KLABU ya Real Madrid imejipanga kumrejesha nyota wake  Achraf Hakimi kikosini akitokea katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
             
 Beki huyo alitolewa kwa mkopo kwenda kujiunga na Dortmund kwa misimu miwili na amekuwa kati ya  mabeki hatari kwa sasa Ulaya.

  Beki huyo anatarajiwa kurejea kwenye kikosi hicho msimu ujao na mkataba wake utaongezwa mpaka mwaka 2025 tofauti na ule wa awali ambao ulitarajiwa kumalizika.

 Rais wa klabu ya Madrid, Florentino Perez amesema staa huyo atapewa mkataba mpaka mwaka 2025 na hii ni baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa Dortmund.

Hata  hivyo kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane kwa sasa yupo kwenye mipango ya kusuka upya kikosi chake ambacho msimu huu kimesuasua kutokana na kuwa na majeruhi wengi. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.