YONO Kevela, Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani Njombe (NJOREFA),amesema kuwa Klabu ya Njombe Mji ipo kwenye hali mbaya kiuchumi kwa sasa hivyo suala la kuwa na mwekezaji ni muhimu.
Njombe Mji inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa inashikilia nafasi ya sita kwenye msimamo kwenye kundi A.
Kevela amesema:-"Timu ipo kwenye hali mbaya kiuchumi na mpira wa sasa ni fedha hivyo ili kuleta ushindani ni lazima kuwe na fedha za kuendesha klabu.
"Unaweza kuwa na wachezaji wazuri lakini ikiwa hakuna fedha inakuwa ngumu kufikia malengo ambayo timu inakuwa imejiwekea," .
Njombe Mji walitangaza kutoa siku saba kwa mtu mwenye nia ya kuwekeza katika klabu hiyo kulingana na masharti waliyoyatoa ikiwemo kitita cha shilingi milioni 300.
Post a Comment