MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wanahitaji kushinda mbele ya Yanga kwa mabao zaidi ya mawili kwa kuwa wanajiamini.
Kesho, Uwanja wa Taifa, saa 1:00 usiku, Ruvu itamenyana na Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kuwatungua kwa bao 1-0 mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, bao pekee la ushindi lilifungwa na Sadat Mohamed.
Bwire amesema kuwa:-"Tupo imara na tunatambua kwamba tutakutana na Yanga ambao nao wapo vizuri hilo halitupi shida, tunaendelea na kampeni yetu ya kupapasa kama ilivyo ada.
"Tumeshinda mchezo wetu kwa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, hatujafurahi kwani ni ushindi mdogo tunapenda kushinda mabao zaidi ya mawili kwani uongozi upo pamoja nasi na wachezaji wanapambana,".
Post a Comment