MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa kinachoibeba timu yake ndani ya Ligi Kuu Bara ni juhudi za wachezaji ndani ya uwanja.

Kagera Sugar iliichapa Mwadui FC mabao 2-1 mchezo wao wa ligi uliochezwa Uwanja wa Kaitaba na kuifanya Kagera Sugar kuwa nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 19.

Maxime amesema:"Wachezaji wanafanya kazi kubwa uwanjani wanastahili pongezi kwani matokeo yanaonekana na mabadiliko makubwa yanaonekana, kwa sasa ni wakati wetu wa kuendelea kujipanga kwa ajili ya mechi zetu za mzunguko wa pili,".

Mzunguko wa kwanza, Kagera Suga ilishinda mechi 10, sare tatu na ilipoteza mechi sita.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.