UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utapambana kupata pointi tatu muhimu mbele ya KMC watakapokutana kesho, Februari,8, Uwanja wa Uhuru.

Azam FC itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kubanwa mbavu na Tanzania Prisons kwa kufungana bao 1-1 mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Uhuru huku KMC ikiitandika bao 1-0 Mbeya City, Samora.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema kuwa wanaitambua vema KMC ni timu imara wataingia kwa tahadhari kubwa.

"Ni timu nzuri KMC ila tutawafuata kwa tahadhari kubwa ili kuona namna gani tutashinda mchezo wetu na kuchukua pointi tatu muhimu," amesema.

Mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru wakati huo KMC ikiwa chini ya Jackson Mayanja na Azam chini ya Ettiene Ndayiragije, Azam ilisepa na pointi tatu muhimu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.