MEDDIE Kagere, kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu, pacha yake na mchezaji mwenzake wa zamani walipokuwa Gor Mahia ya Kenya, Francis Kahata imejibu ndani ya ardhi ya Bongo.

Kagere na Kahata wamehusika kwenye jumla ya mabao 24 yaliyofungwa na Simba kati ya 42 ambayo Simba imefunga msimu huu katika Ligi Kuu Bara wakati timu hiyo ikicheza mechi 19, ikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake 50.

Kagere amefunga mabao 12 na kutoa pasi nne za mabao, huku Kahata akiwa ametupia mabao matatu na kutoa pasi tano.

Jumla wamehusika katika mabao 24. Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck, alisema kuwa furaha yake ni kuona timu inapata matokeo mazuri kwenye mechi zake zote ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

Meddie Kagere amesema kuwa kikubwa kinachowabeba kwa sasa ndani ya ligi ni ushirikiano wao pamoja na juhudi ndani ya uwanja.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.