KITENDO cha kiungo wa Yanga, Mohamed Issa ‘Mo Banka’, kuamua kumvulia jezi namba 8 na kumpatia kiungo wa zamani wa kikosi hicho Haruna Niyonzima baada ya kurejea upya ndani ya klabu hiyo ni wazi amempigia saluti na kumpatia heshima zote.
Niyonzima amerejea Yanga kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa hivi karibuni, akitokea AS Kigali ya kwao Rwanda, baada ya kuachana na Simba ambayo alijiunga nayo msimu mmoja uliopita akitokea Yanga.
Niyonzima ameweka wazi kuwa, baada ya kurejea Yanga fikra na matamanio yake yote, yalikuwa ni kuhakikisha anarejesha jezi yake hiyo namba 8 ambayo aliikuta kipindi hiki ikivaliwa na Mo Banka, hivyo amelazimika kuzungumza naye kwa herufi kubwa hatimaye akakubali kumpatia heshima hiyo.
“Nilipokuja nilianza kuvaa jezi namba 18, kwa sababu ile namba 8 ilikuwa tayari ikimilikiwa na ndugu yangu Mo Banka, lakini ni mshukuru tu kwa kuonyesha heshima kubwa kwangu ya kuamua kunirejeshea kutokana na kujua kuwa ninaipenda jezi hiyo na huwa ni fahari kubwa kwangu nikiivaa.
“Nimpongeze sana Mo Banka kwa kunithamini kiasi hicho maana pamoja na kuvaa jezi namba 18 kwa muda wote niliokuja Yanga, sikuwa na furaha nayo, hivyo ilinipa wakati mgumu sana hadi pale Mo Banka alipotumia heshima yake ya kunirejeshea huku akitambua wazi ninaipenda na jezi hiyo hunipa furaha."
Post a Comment