KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, ameweka wazi kwamba alimtumia mshambuliaji wake, Ditram Nchimbi baada ya straika huyo kumuomba msamaha kufuatia kuondoka kikosini bila ya kumuaga alipotaka kutimkia nchini Misri.

Eymael raia wa Ubelgiji alimtumia straika huyo katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar wikiendi iliyopita baada ya kutomjumuisha katika mechi za Singida United na Prisons.

Nchimbi pamoja na Feisal Salum ‘Fei Toto’ waliondoka kikosini hapo baada ya kupata dili la kwenda kwenye moja

ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Misri, kabla ya dili hilo kuyeyuka. Kocha huyo Mbelgiji ameliambia Spoti Xtra, kuwa; “Nchimbi ni mshambuliaji mzuri hapa kikosini kwetu lakini alikuwa anakaa nje kwa sababu alitaka kwenda Misri bila ya kuwa na ridhaa yangu, ndiyo maana ukaona simtumii.

“Lakini alipoomba msamaha nikaona hakuna namna nikamtumia, na uzuri nilimpa majukumu ambayo alienda kuyafanyia kazi vile ninavyotaka na kutupatia bao katika mechi yetu na Mtibwa.” 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.