OLIVIER Giroud, mshambuliaji wa Chelsea anaweza kuondoka muda wowote kuanzia sasa na kujiunga na klabu ya Inter Milan.
Kocha
Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amethibitisha kuwa kuna uwezekano wa
nyota huyo akasepa ndani ya kikosi cha Chelsea wakati huu wa usajili wa
mwezi Januari.
Vita kubwa ipo mbele ya Newcastle United na Aston Villa ambao nao wanahitaji saini ya Giroud kwa mkopo ili akaungane nao.
Giroud
mwenye umri wa miaka 33 mkataba wake unameguka msimu huu ndani ya
Chelsea na Inter Milan wapo tayari kumpa dili nyota huyo.
Post a Comment