KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vanderbroeck anatarajia kuivunja safu yake ya ulinzi inayoundwa na Muivory Coast, Pascal Wawa pamoja na Erasto Nyoni, kisha kuisuka upya.
Vanderbroeck amefikia hatua hiyo kutokana na kutoridhishwa na uwezo wa mabeki hao katika siku za hivi karibuni na zaidi walipocheza dhidi ya Namungo FC, juzi Jumatano. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar, Simba ilishinda 3-2.
“Kuna makosa mengi ya kiufundi ambayo yamekuwa yakifanywa na safu yangu ya ulinzi kwa upande wa mabeki wa kati na kujikuta tukifungwa mabao ambayo unaweza kuyaita kuwa ni mepesi.
“Nitafanya mabadiliko na kuna uwezekano katika mechi yetu ijayo dhidi ya Costal Union nikawapana nafasi mabeki wengine,” alisema Vandenbroeck na kuongeza kuwa.
“Katika mechi nne tulizocheza hivi karibuni, licha ya kushinda lakini tumekuwa tukiruhusu mabao.”
Matokeo ya mechi hizo ni: Mbao 1-2 Simba, Alliance 1-4 Simba, Simba 2-1 Mwadui na Simba 3-2 Namungo
Post a Comment