UONGOZI wa Simba leo umetoa tamko rasmi kuhusu suala la mchezaji wa Yanga, Ramadhan Kabwili, kudai kwamba aliahidiwa kupewa gari aina ya Toyota IST ili asicheze kwenye mchezo wa watani wa jadi msimu uliopita 2018/19.

Kabwili, aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha radio ambapo alidai kuwa alifuatwa na Simba ili afanye makusudi kupata kadi ya njano kwenye mechi yake dhidi ya JKT Tanzania ili asicheze mbele ya Simba.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Simba kupitia ukurasa wa Istagram imeeleza kuwa wanasikitishwa na kauli ya mchezaji huyo wa Yanga, Ramadhani Kabwili kwa kuishushia hadhi klabu ya Simba ambayo inazidi kujijenga kwa sasa kwenye ushindani wa soka.

"Tumepokea taarifa ya Ramadhan Kabwili wa Yanga aliyoitoa kupitia kipindi cha Radio cha East Afrika, kwa masikitiko Januari 27, ni za kusikitisha kuhusu upangwaji wa matokeo, kauli ambayo inapingwa na klabu ya Simba na kukemewa vikali.

"Tunashukuru kwa hatua iliyochukuliwa na TFF kwa kuchukua hatua na inaamini kwamba ipo kwenye yombo husika na vitachukua hatua stahiki.

"Kwa sasa klabu inawekeza nguvu nyingi kwenye mechi za Kombe la Shirikisho, ligi kuu pamoja na mashindano mengine," ilieleza taarifa hiyo.

Simba kesho itashuka kesho Uwanja wa Taifa kumenyana na Namungo mchezo wa Ligi Kuu Bara

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.