IDD Cheche, Kocha Msaidizizi wa Azam FC amesema kuwa wanahitaji kulirudisha kabitini Kombe la Shirikisho hivyo watapambana leo mbele ya Friend Rangers, Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema mechi za Shirikisho ni zaidi ya fainali kutokana na ugumu wake ulivyo.
“Mechi hizi ni ngumu kwani ni zaidi ya fainali hasa ukizingatia kwamba ukipoteza na safari yako inaishia hapo, tutaingia uwanjani kwa tahadhari kwa kuwa wapinzani wetu ni timu bora nasi tunahitaji kutetea kombe letu.
“Kikubwa ni kuona kwamba wachezaji wanafanya kazi yao kwani maandalizi yapo vizuri nasi tunaamini tutafanya vizuri mashabiki watupe sapoti,” amesema Cheche.
Post a Comment