HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wamemuita mlinda mlango wao, Ramadhani Kabwili baada ya kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa Simba kuwa walitaka kumpa rushwa apate kadi ya njano ili asicheze mchezo unaofuata dhidi ya mabingwa hao msimu uliopita.
Kabwili aliongea na kituo kimoja cha radio, jijini Dar es Salaam kuwa viongozi wa Simba walimuahidi kumpa gari aina ya IST kama angepata kadi ya njano ili asiwepo kwenye mechi dhidi yao ingawa mwenyewe alikataa.
Bumbuli amesema hilo ni suala la jinai, wamemuita mchezaji huyo ili kuwapa ushahidii ambao wataupeleka kwenye vyombo vya usalama kwa ajili ya hatua za kisheria.
"Hili ni suala la jinai hivyo tumemuita Kabwili atupe ushahidi ili tupeleke kwenye vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki," amesema
Post a Comment