KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anashangazwa na mtindo wa nyota wake Bernad Morisson kuendelea mtindo wake wa kucheza na mpira 'Shibobo' licha ya kumzuia asifanye hivyo.
Morrison alianza kuonyesha makeke yake kwenye mchezo wake wa kwanza mbele ya Singida United ambapo alicheza na mpira kwa kutembea juu na kupiga pasi alifanya hivyo tena jana mbele ya Tanzania Prsons Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa mtindo anaoufanya Morisson ni hatari kwa afya yake kwani ni kitu ambacho amekuwa akimzuia.
"Morrison ni mbabe sana, nilimzuia aache kuchezea mpira ila nimeona amerudia tena hili jambo nitakaa naye kuzungumza naye tena kwa mara nyingine kwani hanifurahishi mimi na ataigharimu timu," amesema.
Kwenye ushindi wa mabao 2-0 walioupata Yanga, Morison alifunga bao moja kwa penalti na alitoa pasi ya bao lililofungwa na Yikpe

Post a Comment