LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa nyota wake, Yikpe Gnamien anaingia kwenye mfumo taratibu ni suala la muda kurejea kwenye ubora.

Kwenye ushindi wa jana mbele ya Prisons wa mabao 2-0 walioupata Yanga, Uwanja wa Uhuru mchezo wa Kombe la Shirikisho, Yikpe alifunga bao la pili akimalizia pasi ya Bernard Morrisons.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eyamel amesema kuwa anamuona akiwa uwanjani Yikpe ni mtu mwenye juhudi jambo ambalo linamfanya azidi kumpa mbinu tofauti.

"Ni mchezaji ambaye anakuja vizuri kwani akiingia uwanjani anafanya kile ambacho ninamwelekeza na vingine anavijua mwenyewe ni kitu kizuri kuona anapata nafasi.

"Bado wapo wachezaji wengi ambao wanaweza na watapata nafasi kwani hakuna mwenye namba ya kudumu ndani ya Yanga," amesema,

Baada ya kupenya hatua ya 32 bora, Yanga mchezo wake unaofuata kwenye hatua ya 16 bora itakuwa dhidi ya Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.