UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa, timu ya Sahare Stars sio watu wazuri kwani walikaza mwanzo mwisho kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Januari, 25, Uwanja wa Gairo.

Mtibwa Sugar ilianza kupachika bao la kuongoza kipindi cha pili kupitia kwa Awadh Salim dakika ya 64 bao lake lillisawazishwa na  Hussein Amir dakika ya 83 na kufanya dakika 90 zikamilike kwa sare ya kufungana bao 1-1. 

Sare hiyo ya kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora iliwapelekea wapigiane penalti ambapo Sahare Stars ilishinda kwa penalti 3-2 walizopata Mtibwa Sugar.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wapinzani wao sio watu wazuri kwani walikamia mechi mwanzo mwisho.

"Tulicheza mpira kwa hesabu na ukizingatia kwenye Shirikisho ni pigo moja tu unakwenda nje, kwa kufungwa ndani ya dakika tisini tulikomaa na wapinzani wetu walitukamia na kutufanya tupoteze kwa changamoto ya penalti," amesema.

Sahare Stars imepenya hatua ya 16 bora na itamenyana na Panama FC

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.