HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa timu ya Namungo amesema kuwa leo ataingia na mbinu mpya itakayompa nguvu ya kupata pointi tatu kwenye mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Taifa, saa 1:00 Usiku.
Namungo iliyo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 16 itamenyana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 41 baada ya kucheza mechi 16.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa moja ya mpango mkubwa wa timu yake ni kupata pointi tatu mbele ya Simba ili kuwajengea wachezaji wake hali ya kujiamini.
“Mchezo wetu utakuwa mgumu na wenye ushindani, unapocheza na bingwa lazima uwe na tahadhari kabla hajakuumiza tunalitambua hilo na tutaingia uwanjani kwa tahadhari tukiwa na malengo ya kuzipata pointi tatu muhimu mashabiki watupe sapoti,"amesema.

Mechi iliyopita Namungo ilishinda mabao 3-2 mbele ya Prisons Uwanja wa Samora huku Simba ikishinda mabao 4-1 mbele ya Alliance Uwanja wa CCM Kirumba.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.