STRAIKA ghali zaidi Afrika Mashariki, Mbwana Samatta, Jumanne ijayo anaanza kukipiga ndani ya klabu yake mpya ya Aston Villa.

Habari za mchezaji huyo kukinukisha ndani ya uzi wa Aston Villa, kimeamsha mzuka mkubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaamini kwamba atawaokoa na kumaliza mchezo huo kutoka na ubora na rekodi zake.

Siyo mashabiki wa Villa ndani ya Ulaya tu, hata Watanzania wanatamani kuona mchezaji huyo akianza kucheza ndani ya ardhi ya England baada ya kumuombea dua kwa miaka mingi.

Nahodha huyo wa Taifa Stars, amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne na nusu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji ambayo mashabiki wake walimwaga machozi ya huzuni waliposikia kipenzi chao ameuzwa lakini walimuaga kwa heshima.

Kwa mujibu wa Skysports, mchezaji huyo mwenye miaka 27, atakuwa tay City, Jumanne saa 4:45 usiku pale Villa Park katika mechi ya Kombe la Ligi.

Kwa mujibu wa kituo hicho maarufu Samatta ndani ya muda huo atakuwa tayari na vibali vyote mkononi na kanuni zitakuwa wazi.

Katika mechi ya awali ya Kombe la Ligi, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 hivyo wenyeji wanaombea Samatta akichafue Jumanne.

Kama Aston Villa wakishinda, watacheza na mshindi dhidi ya Manchester City na Man United kwenye fainali ya michuano hiyo maarufu itakayopigwa Machi 1, mwaka huu pale Wembley.

Samatta amekuwa gumzo kwenye vyombo vya Habari vya Ulaya baada ya kuandika rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu ya England.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.