KOCHA wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars) na Yanga, Marcio Maximo amesema kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji kama Mbwana Samatta, lakini wanakosa misingo
bora ya kuwaibua.
Maximo ambaye aliifundisha Taifa Stars kuanzia mwaka 2006 mpaka 2010 amliyasema hayo kutokana na mafanikio ya Samatta, ambaye anajivunia kwa kuwa kocha wa kwanza kumuita kuichezea timu ya Taifa.
Kocha huyo ambaye sasa anaifundisha timu ya taifa ya Guyana alisema kuwa pamoja na kupata shutuma nyingi za kuwaita wachezaji chipukizi Taifa Stars, aliziba masikio na kuendelea na mfano wake.
Maximo alisema kuwa Samatta ambaye kipindi anamjumuisha Taifa Stars alikuwa chini ya miaka 20, alifanikiwa kumjenga kwa misingi ya uchezaji na sasa kufikia hapa alipo.
Alisema kuwa mbali ya Samatta wakati huo alikuwa akichezea timu ya African Lyon, katika kikosi chake pia kilikuwa na wachezaji wengine vijana kama Jerryson Tegete, Mrisho Ngassa, Yusuph Soka, John Bocco, Kigi Makasi na Himid Mao.
Alifafanua kuwa Samatta alikuwa na kipaji cha hali ya juu pamoja na ushindani wa namba ndani ya Taifa Stars. Kwa mujibu wa Maximo, wadau wengi wa soka walilalamika kuwa wachezaji wengi vijana hawakuwa na timu za Ligi Kuu au Daraja la Kwanza na kuamini kuwa hawataweza kuisaidia timu hiyo.
“Mipango yangu ilikuwa ya baadaye na wala haikuwa ya wakati ule, baadaye walianza kuona matunda, ambapo wachezaji wote walikuwa nyota na kutakiwa kimataifa,
“Samatta alikuwa na kipaji kikubwa pamoja na baadhi ya watu kupinga, hata hapo alipojiunga na Simba, alikuwa na kipaji na kucheza nusu msimu na baadaye kujiunga na timu ya TP Mazembe,” alisema Maximo.
Alisema kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, lakini wanashindwa kupata mafunzo ya kisasa ili kuwezakucheza kimataifa.
Alisema kuwa amekaa Tanzania miaka mitano na kuona jinsi gani anaweza kuwasaidia wachezaji vijana
Post a Comment