KOBE Bryant, aliyekuwa mchezaji nyota wa mpira wa kikapu ambaye alikuwa akiwakilisha vizazi vingi vya mchezo huo amefariki kwa ajali ya helkopta iliyotokea jana, Jumapili, Januari,26.
Nyota huyo wa zamani wa timu ya Los Angeles Lakers alikuwa kwenye helkopta hiyo binafsi ilipopata ajali na imethibitishwa kwamba alikuwa na mwanaye wa miaka 13 wote walifariki baada ya kutokea kwa ajali hiyo maeneo ya Calabasa, California.
Watu wengi mashuhuri wamemlilia nyota huyo ikiwa ni pamoja na Raheem Sterling Neymar Jr, Tom Brady, Usain st Leo Bolt , Gareth Bale, Mohamed Salah na Marcus Rashford kupitia mitandao ya kijamii kwa kuandika maneno ya kumuombea kheri.
Kobe alizaliwa Agosti, 23 1978 na kufariki mwaka 2020, kwenye maisha yake ya kucheza mpira wa kikapu alishinda mataji matano ya NBA na kwenye orodha ya wafungaji Bora wa muda wote anashika nafasi ya nne akiwa na jumla ya pointi 38,387

Post a Comment