UONGOZI wa azam FC umesema kuwa leo utaingia kwa tahadhari kubwa kumenyana na Friend Rangers kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho.
Azam FC itashuka Uwanja wa Uhuru, leo, Januari 27 ikiwa ni hatua ya 32 bora.
Idd Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wataingia uwanjani kwa tahadhari ili kutofanya makosa yatakayowapotezea nafasi ya kusonga mbele.
"Nidhamu ni silaha kubwa kwa wachezaji pamoja na ushirikiano, imani yetu ni kwamba timu tunayocheza nayo ni bora ndio maana ipo hatua hii ambayo sisi tupo kikubwa ni tahadhari tusifanye makosa yatakayotugharimu.
"Mpira ni mchezo wa makosa ila tumefanyia kazi makosa yetu ili kuwa kwenye ushindani, ukizingatia kwamba sisi ni mabingwa watetezi," amesema
Post a Comment