KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude, amesema watajituma hadi tone la mwisho kuhakikisha wanabeba Kombe la FA msimu huu baada ya mwaka jana kutolewa hatua za awali.
Simba inacheza Jumamosi hii dhidi ya Mwadui katika mchezo wa FA kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar.
Aidha kikosi cha Simba tayari kimeshaingia kambini katika Hoteli ya Ndege Beach, Dar ambapo ndipo wameweka kambi ya kudumu hadi mwishoni mwa msimu.
Mkude alisema wamejiandaa kuona wanafanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa kombe hilo.
“Tumeji-andaa vyema chini ya kocha wetu Sven kuweza kufanikiwa kushinda mchezo wetu dhidi ya Mwadui ili kupata pointi tatu, tutapambana ili kuona tunashinda katika kila mechi tutakayocheza japokuwa wapinzani wetu nao watakuwa wamejiandaa.
“Lengo ni kuona tunafanikiwa kutwaa Kombe la FA pamoja na ligi kuu,” alisema Mkude.
Post a Comment