KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael amesema amechukizwa na kitendo cha mshambuliaji wa timu hiyo, Ditram Nchimbi kwenda Misri kufanya majaribio huku akifanya udanganyifu mkubwa.
Inadaiwa kuwa Nchimbi na kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Feitoto’ waliondoka nchini kuelekea Misri kufanya majaribio katika Klabu ya Smouha inayoshiriki Ligi kuu ya Misri lakini kocha huyo haamini kama kweli walienda kufanya majaribio kwenye timu hiyo kwa kuwa haina nafasi kwa wachezaji wa kigeni.
Eymael alisema kuwa, hakufurahishwa na kitendo cha Nchimbi kumdanganya na kuondoka bila ya ruhusa yake hivyo atahakikisha anachukuliwa hatua za kinidhamu na uongozi wa juu wa timu hiyo. “Ni kweli Nchimbi aliondoka yeye na Feisal lakini haikuwa ni ruhusa yangu hasa kwa Nchimbi kwa sababu Feisal alikuwa na ruhusa tayari ila siyo kwa Nchimbi, amenidanganya.
“Nilimpigia mmoja kati ya makocha wa Misri kutaka kujua ukweli, amenieleza kwamba kuna timu mbili lakini moja ambayo ni Smouha haikuwa ikihitaji wachezaji wa kigeni kwa kuwa hakuna nafasi.
“Lakini Nchimbi aliendelea kusisitiza kwamba wakala wake wa Nigeria ndiye amemueleza huo ujinga ndiyo maana nasema ni muongo kwani nilimuuliza kabla, sasa siyo jambo zuri kwenye timu na siwezi kulifumbia macho nitalipeleka kwa uongozi ili uchukue hatua,” alisema Eymael
Post a Comment