BAADA ya Mtibwa Sugar kutupwa nje kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho na Sahare Stars kwa kufungwa penalti 3-2 baada ya sare ya kufungana bao 1-1, Uongozi wa Mtibwa umesema kuwa hasira zote zitaishia kwa Azam FC kesho.
Januari,30, Mtibwa Sugar iliyo chini ya Zuber Katwila itamenyana na Azam FC ikiwa na kumbukumbu ya kuondolewa kwenye kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora huku Azam FC ikitinga hatua ya 16 kwa kuichapa Friend Rangers mabao 3-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, amesema kuwa wamesahau maumivu ya kufungwa na Sahare Stars akili zote ni kwa Azam FC.
“Tutakuwa na kazi ya kucheza na Azam FC mchezo wa ligi, habari za Shirikisho tayari zimeshafungwa, tutamaliza hasira zetu kwa kupata matokeo mazuri, mashabiki watupe sapoti katika hili,” amesema Kifaru.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 10 ikiwa imecheza mechi 16 na ina pointi 22 itakutana na Azam FC Uwanja wa Uhuru ambayo ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 16 na ina pointi 35.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.