Beki kisiki wa Simba, Erasto Nyoni amemaliza mkataba na mabingwa hao na kuweka wazi kuwa hatma yake itajulikana baada ya Afcon, Misri.


Mwanaspoti limedodosa na kubaini sababu iliyomfanya ashindwe kuongeza mkataba mpya kuwa ni kutaka kwenda kuboresha thamani yake katika mashindano ya Afcon yanayotarajiwa kuanza mwezi Juni nchini Misri.


Chanzo cha ndani kutoka kwa rafiki yake wa karibu wa mchezaji huyo kililiambia www.mwanaspoti.co.tz kuwa Simba iliweka mezani sh40 milioni na mshahara wa Sh2milioni kwa mwezi ili kumuongeza mkataba nyota huyo.


Pamoja na dau hilo taarifa zinasema Nyoni anajifikiria na kama ataona ni sawa anasaini akitoka Afcon.


"Nyoni hadi sasa ajamalizana na Simba sababu ni kupewa kiasi kidogo cha fedha ambacho uongozi wa Simba umesema kinaendana na thamani yake hivyo amesema anataka akapandishe thamani Afcon na endapo atapata timu nyingine basi atatokomea huko."


"Sijajua anataka kiasi gani, lakini amesema kiasi alichowekewa na Simba ni kidogo kutokana na kazi kubwa aliyoifanya msimu huu na kuweka wazi kuwa wanaona thamani yake ni ndogo basi anaomba akaiongeze katika mashindano ya Afcon akirudi kama atakuwa tayari kusaini atafanyaivyo," kilidai chanzo hicho

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.