Baada ya kuonyesha vitu adimu vilivyomkosha kila Mwanayanga na kuwaumiza wapinzani, straika wa Yanga, Bernard Morrison, ameingia chimbo kutengeneza dawa ya mabeki jeuri.

Morrison aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo, amekuwa gumzo kutokana na mbwembwe zake za kuchezea mpira maarufu kama Shobobo.

Katika mechi mbili pekee alizocheza dhidi ya Singida United na Tanzania Prisons, tayari amedhirisha kuwa na kiwango bora, kwani pamoja na kutoa burudani, ameisadia timu yake kupata ushindi.

Sasa kwa taarifa yao wale wanaumizwa na miondoko yake uwanjani, wajiandae kuona vitu vingine vipya na safari hii mabeki wajipange.

Baada ya michezo miwili aliyocheza, Morrison amebaini kuna mabeki wabishi na watamkamia katika mechi zijazo, hivyo ameamua kujifungia ndani kupitia video za michezo yote ya timu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Morrison ameeleza kuwa kwa kipindi walichopewa mapumziko, anakuwa bize kuangalia video za mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara ili kubaini aina ya uchezaji wa mabeki atakaokabiliana nao.

“Nimeona ni vizuri kupitia video za timu nitakazocheza nazo, nipate vitu vitavyonisaidia uwanjani, najua safari hii mabeki watakuwa wamejipanga kukabiliana na mimi,’ alisema winga huyo raia wa Ghana.

Katika mechi mbili alizocheza, nyota huyo wa Yanga amefunga bao moja na kutengeza nafasi za mabao mawili ‘assists’. 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.